Mamlaka na Miradi

MAMLAKA NA ENEO LA KIUETENDAJI LA CHAVITA

Ufafanuzi kuhusu mamalaka ya CHAVITA umetolewa katika katiba ya CHAVITA. Sheria za nchi pia zimetoa ufafanuzi kuhusu mipaka na maeneo ya kiutendaji kwa kuzingatia wa maadili na utamaduni wa nchi yetu. Katiba ndiyo msingi mkuu wa CHAVITA na inaundwa na vyombo vitatu vinavyoongozwa na Viziwi wenyewe ambavyo ni Mkutano Mkuu,Mkutano wa Kamati Kuu ya Utendaji na Mkutano wa Sekretarieti. Mkutano mkuu ndicho chombo chenye mamlaka ya juu. Kamati Kuu ya Utendaji ni chombo cha usimamizi wa shughuli za kila siku na Sekretarieti ikiwa chini ya usimamizi wa Mkurugenzi Mtendaji ina wajibu wa kupanga na kutekeleza mipango na shughuli za chama. Kwa sasa CHAVITA kinaendesha shughuli zake katika maeneo makuu yafuatayo:

Maeneo ya Programu

Ushawishi na Utetezi
Kupunguza umasikini
Lugha ya Alama
Jinsia na watoto
Mahusiano ya umma na uanachama
Afya na Ustawi wa Jamii

CHAVITA kinaendesha jitihada za kukuza uelewa na kujenga heshima kuhusu haki za kisheria na za binaadamu kwa Viziwi. Mpango huu unafanikishwa kwa kuwahamasisha na kuwajengea uwezoViziwi wenyewe, kuhamasisha jamii ,taasisi na serikali. Jitihada za utetezi unaofanywa na CHAVITA kwa kawaida zinalenga kuhakikisha kuwa sheria, sera na utekelezaji wake zinawanufaisha Viziwi.

CHAVITA kinajenga uwezo wa kiuchumi kwa kuwaunganisha Viziwi na vyanzo vya mitaji, kutoa mafunzo na kuwezesha shughuli za ujasilimali kwa kushirikiana na wadua wengine.

Programu hii inalenga kukuza uelewa na matumizi ya Lugha ya Alama ya Tanzania(TSL) kwa Viziwi na wasio Viziwi. Mafanikio ya Programu hii yanapatikana kupitia mafunzo ya Lugha ya Alama ya Tanzania,uratibu wa huduma za ukalimani, kufanya tafiti na utengenezaji wa kamusi ya Lugha ya Alama ya Tanzania na machipisho mengine muhimu.

Jukumu la idara hii ni kuweka vipaumbele na ujumuishi wa masuala ya jinsia katika programu zilizopo ndani ya CHAVIA, kuwawezesha na kuwapa stadi wanawake Viziwi,kuwahamsisha wanawake Viziwi kuhusu haki na thamani waliyonayo: wanawake Viziwi hujengewa uwezo kupitia mafunzo na ushauri kuhusu ongezeko la thamani katika huduma na bidhaa wanazozalisha ,kuwaunganisha na vyanzo vya mitaji na kuhimiza uendeshaji miradi ya ubunifu.

Idara hii ina jukumu la kuweka msingi imara wa uanachama kupitia uhamasishaji wa Viziwi , kuhakikisha wanashiriki kamilifu katika kuunda mikakati ya utatuzi wa matatizo yanayowakabili na kutetea haki zao. Idara hii inahusika na mahusiano ya kijamii na taarifa za uenezi na uhamasishaji.

Idara hii ina wajibu wa kuwawezesha ujumuishi wa Viziwi katika masuala ya kiuchumi kwa kuwaunganisha Viziwi katika fursa za ajira,kuwapa ushauri ,kuwaunganisha na huduma ya upimaji wa masikio na kuhakikisha watoto Viziwi wanasajiliwa shuleni.

Mhutasari wa Miradi

Viziwi ni sehemu ya uanuwai wa kibinaadam ,wanakabiliwa na changamoto katika kufikia haki za binaadam. Nchini Tanzania viziwi wanaishi katika hali duni kutokana na vikwazo vya kijamii, kiuchumi ,kimtazamo na kisheria amabvyo kwa ujumla kuzuia ushirikishwaji wao kajamii katika nyanja mbalimbali za maisha na pia kutonufaika na au kufikia haki za msingi za binaadamu na kwa uhuru kama ilivyo kwa wanajamii wengine.

Kwa sasa,haki za viziwi zimebainishwa katika mkataba wa kimataifa wa haki na fursa kwa watu wenye ulemavu(UNCRPD),sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004,sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 na sera ya taifa ya elimu ya mwaka 2014. Mradi huu unashughulikia suala la serikali za mitaa kujikita katika uundaji wa mipango ujumuishwaji na ya makusudi ya kuhakikisha kuwa jamii ya viziwi inapata haki sawa na fursa ya kushiriki kikamlifu katika michakato ya serikali za mitaa na uwajibikaji umma.

Sera, sheria,program na huduma zote zinahitaji kuzingatia mahitaji ya viziwi ikiwa ni suala la haki na si la kihisani. Mradi unaendeshwa Arusha mjini katika eneo la kaskazini mwa Tanzania jirani na mkoa wa kimanjaro ambako jamii ya viziwi wa Kimaasai wanaishi. Tamkakati wa mradi ni kutoa mafunzo bora ya kujenga mwamko na kutoa stadi za utetezi ili kuwezesha kutekelzwa kwa sharia za kimataifa na za kitaifa. mradi utafanya kazi kwa kuwashirikisha maofisa wa serikasli ngazi ya kata jijini Arusha kwa kuwapa mafunzo kuhusu haki za viziwi amabzo zinaweza kufikiwa kutokana na mipango ya ujumuishwaji.

Jambo hili litawezesha viziwi kushiriki kikamilifu katika michakato ya serikali za mitaana uwajibakaji kwa umma. viziwi wa jamii ya Kimaasai wapatao 25 watanufaika na mradi huu kwa kutambua haki zao kama zilivyoanishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, sharia zinahusu masuala ya watu wenye ulemavu katika ngazi za kitaifa na kimataifa na yaliyomo katika mfumo wa micahalkato ya serikali za mitaa na uwajibikaji kwa umma

Mradi utakapohitimishwa utawawezesha wanufaikaji kuwa wakufunzi kwa ajili ya kuwafundisha viziwi wengine hapo mkoani.


  • Mradi wa Kupunguza Umasikini
    Malengo ya mradi huu ni kuimarisha hali ya kujitegemea kwa jamii ya viziwi nchini Tanzania na hasa wanawake na vijana,mradi unalenga mikoa saba ya tnzania bara anmbayo ni Kagera, Kigoma, Singida, Mtwara, Lindi, Kilimanjaro na Arusha.

  • Mradi wa mafunzo ya Lugha ya Alama na Utetezi Tanzania.
    Lengo la mradi huu ni kuimarisha na kuendeleza lugha ya Alama ya Tanzania katika ngazi za wilaya kwa kutoa mafunzo kwa wakunzi wa Lugha ya Alama, viziwi, wazazi wa watoto viziwi na watoa huduma..
  • Mradi Wahaki ya Afya ya Uzazi kwa Vijana
    Mradi huu unalenga kuhamasisha vijana viziwi wa kike na wakiume walio na umri wa miaka 10 hadi 20 kuhusu haki afya ya uzazi na kuwapa stadi za maisha za kupambana na UKIMWI na umasikini.


VIPAUMBELE NA MAHITAJI YA CHAVITA KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO (2017-2020)

MAENEO YA KIPAUMBELE KATIKA KAZI MATAWI YALIYOPO KATIKA NGAZI YA MSINGI.
1 Mafunzo na uendelezaji wa viongozi na watumishi wa CHAVITA 1. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Morogoro
2. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Tanga
3. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Mwanza
4. CHAVITA -Tawi la Mkoa wa Ruvuma
5. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Arusha
6. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Shinyanga
7. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Dodoma
8. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Dar es salaam
9. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Pwani
10. CHAVITA- Tawi la Mkoa wa Mtwara
11. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Tabora
12. CHAVITA- Tawi la Mkoa wa Mara
13. CHAVITA- Tawi la Mkoa wa Kagera
14. CHAVITA- Tawi la Mkoa wa Iringa
15. CHAVITA - Tawi la Mkoa wa Mbeya
16. CHAVITA- Tawi la Mkoa wa Kigoma
17. CHAVITA- Tawi la Mkoa wa Kilimanjaro
2 Kujenga uwezo wa ugemaji rasilimali katika ngazi ya makao makuu na katika matawi ya CHAVITA .
3 Kujenga uelewa na kuhamasisha wadau mbalimbali kuhusu haki na mambo muhimu yanayowaathiri viziwi.
4 Kuendeleza Lugha ya Alama ya Tanzania.
5 Kujenga uwezo wa kiuchumi kwa Viziwi katika ngazi ya matawi.
6 Kujenga uelewa na kuhamasisha wadau mbalimbali kuhusu haki na mambo muhimu yanayowaathiri viziwi.
7 Kushawishi utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa haki na ursa kwa watu wenye ulemavu( UNCRPD), Malengo ya maendeleo(SDG) na mkataa wa kimataifa wa haki za binaadamu kuhusu haki za watu wenye ulemavu hususani viziwi na Lugha ya Alama.
8 Kuimarisha ufikikaji wa elimu kwa viziwi kupitia mfumo wa elimu wa matumizi ya Lugha mbili
9 Kuwawezesha viziwi kushiriki katika maendeleo ya kijamii kwa kukomesha unyanyapaa.