• Kuwezeshana na Kuboresha Hali
    za Maisha ya Viziwi
    Matumizi ya Lugha ya Alama miongoni mwa viziwi na watu wasio na uziwi
    CHAVITA kinajenga uwezo wa kiuchumi kwa kuwaunganisha Viziwi na vyanzo vya mitaji, kutoa mafunzo na
    kuwezesha shughuli za ujasilimali kwa kushirikiana na wadua wengine.
  • Harambee..!!
    Ili kufikia malengo yetu CHAVITA kinaomba mchango wa wasamlia wema,
    watu binafsi,taasisi, taasisi za zinazotoa ufadhiri popote ili mkuwezesha
    utekelezaji wa sghuli zetu ambazo zina matokeo ya mabadiliko makubwa
    katika maisha ya viziwi ndani ya Jmhuri ya muungano wa Tanzania.
chavita-donate

Tembelea wavuti wa alama za lugha ya viziwi hapa

Kuboresha Hali za Maisha ya Viziwi

Mara nyingi viziwi huwa na vipato vidogo vilivyo chini ya mstari wa umasikini na hawana rasilimali za kuweza kujikinga na majanga na kukabiliwa na athari za kijamii na kiuchimi..

Elimisha Viziwi Nchini Tanzania

Mara nyingi viziwi huwa na vipato vidogovilivyo chini ya mstari wa umasikini , hawana rasilimali zinazoweza kutumika kukabili majanga, wana hali duni kijamii na kiuchumi, wana elimu duni, wana hali duni za afya na rishe duni,hawanufaiki na huduma na ulinzi wa kijamii, wanatengwa, wanabaguliwa na kunyimwa haki ya kutumia Lugha yao wenyewe.

Maendeleo ya Lugha ya Alama

Program hii inalenga kuongeza uelewa na matumizi ya Lugha ya Alama ya Tanzania (LAT)miongoni mwa viziwi na watu wasio na uziwi. program hii inaendeshwa kupitia utoaji wa mfunzo ya Lugha ya Alama,uratibu wa huduma za ukalimani wa Lughya Alama, kuendesha tafiti na uandaaji wa kamusi na nyenzo zingine.

Miradi ya Karibuni

  • Mradi wa Kupunguza Umasikini
    Malengo ya mradi huu ni kuimarisha hali ya kujitegemea kwa jamii ya viziwi nchini Tanzania na hasa wanawake na vijana,mradi unalenga mikoa saba ya tnzania bara anmbayo ni Kagera, Kigoma, Singida, Mtwara, Lindi, Kilimanjaro na Arusha.

  • Mradi wa mafunzo ya Lugha ya Alama na Utetezi Tanzania.
    Lengo la mradi huu ni kuimarisha na kuendeleza lugha ya Alama ya Tanzania katika ngazi za wilaya kwa kutoa mafunzo kwa wakunzi wa Lugha ya Alama, viziwi, wazazi wa watoto viziwi na watoa huduma..
  • Mradi Wahaki ya Afya ya Uzazi kwa Vijana
    Mradi huu unalenga kuhamasisha vijana viziwi wa kike na wakiume walio na umri wa miaka 10 hadi 20 kuhusu haki afya ya uzazi na kuwapa stadi za maisha za kupambana na UKIMWI na umasikini.