Kuhusu Sisi

CHAVITA ni asasi iliyosajiliwa ndani ya Jamhuri ya muuganao wa Tanzania , CHAVITA kiliundwa na viziwi wenyewe mnamo mwaka 1984 kwa madhumuni ya kufikia jamii yenye usawa na haki kwa viziwi.Makao makuu ya CHAVITA yako jijini Dar es Salaam na kikiwa na matawi 17 katika ngazi ya mikoa. Lengo letu ni kuboresha hali ya maisha ya jamii ya viziwi kupitia shughuli za utetezi ili kufikia usawa na haki za binaadamu kwa jamii ya viziwi na kukuza na kuendeleza Lugha ya Alama ya Tanzania.

Dira na Dhamira Yetu

Dhamira
Kuimarisha na kuendeleza ufikikaji wa haki zote za bianaadamu na za kiraia miongoni mwa viziwi wa Tanzania na kupigania kupunguzwa na kuondolewa kwa vikwazo vyote vinavyozuia ushiriki wao katika haki hizo ili viziwi wawezekutimiza malengo yao,kuboresha viwango vya maisha na kuchangia maendeleo katika jamii.

Dira
Kuwa na jamii ya Viziwi iliyowezeshwa na iliyo makini na jamii ya watanzania yenye mazingira wezeshi kwa Viziwi katika kufikia na kunufaika na haki zao,kukamilisha malengo yao na kuchangia maendeleo katika jamii.

Lengo Kuu
Kuboresha hali ya maisha ya Viziwi wa Tanzania bara kwa kutekelezaji haki za binaadamu na za kiraia.”

Madhumuni ya Msingi
Kuimarisha uwezo wa CHAVITA na wanachama wake wa kukuza na kuendeleza viwango vya hali ya maisha.

Maelezo ya uhitaji

Mara nyingi viziwi nchini Tanzania hutengwa na kukabiliwa na vitendo vya unyanyapaa ndani ya jamii na hivyo kuwa jamii masikini zaidi, wanawake na watoto viziwi ndiyo hasa hukabiliwa na hali duni zaidi. Mara nyingi viziwi huwa na vipato vidogovilivyo chini ya mstari wa umasikini , hawana rasilimali zinazoweza kutumika kukabili majanga, wana hali duni kijamii na kiuchumi, wana elimu duni, wana hali duni za afya na rishe duni,hawanufaiki na huduma na ulinzi wa kijamii, wanatengwa, wanabaguliwa na kunyimwa haki ya kutumia Lugha yao wenyewe.

Amali za CHAVITA

Kuheshimu Utashi wa walengwa
Kujituma
Mawasiliano
Kujenga uwezo
Ushirikiano
Ubunifu na Maendeleo
Kuheshimiana

Kuwaunga mkono na kuwawezesha Viziwi ,kuheshimu haki ya kila mmoja katika kutoa maamuzi na kufikia malengo yake,kutoa uelekeo wa programu na huduma. Chama kimejipanga kuzingatia masuala ya msingi kwa Viziwi na kuandaa huduma na ushirikiano unaohitajika kwa viziwi.

Kuwasaidia na kuwawezesha walengwa kufikia maamuzi sahihi na kuweza kufikia malengo yao binafsi na ya taaluma zao.

Ni imani yetu kuwa suala la mawasiliano ni changamoto ambayo chama kinatakiwa kushughulikia. Lengo ni kuhakikisha kuwa viziwi wanajimudu kimawasiliano kuweza kuchangamana kikamilifu katika jamii. Kwa hiyo chama kinakusudia kukuza,kuendeleza na kufanya utetezi wa matumizi na kukubalika kwa Lugha ya Alama ya Tanzania.

Kuendeleza jitihada za kuweka mazingira wezeshi kwa Viziwi kuwa na maamuzi huru juu ya maisha yao.

Tunatambua na kushukuru michango ya wadau mbalimbali inaoyotolewa kwa njia mbalmbali katika kufanikisha kazi zetu. Tumejipanga kutekeleza ahadi zetu na kuendeleza uaminifu miongoni mwetu na kwa wadau wetu.

Tumeamua kundelea kufanya maboresho katika kila jambo tunalolifanya na kuzingatia ubunifu kuleta ubora na mafanikio zaidi katika kufikia utume na dira yetu.

Msingi mkuu wa mafanikio ya amali zetu ni kuheshimiana kati na miongoni mwa Viziwi na kati ya Viziwi na jamii kwa ujumla.