Mara nyingi viziwi huwa na vipato vidogo vilivyo chini ya mstari wa umasikini na hawana rasilimali za kuweza kujikinga na majanga na kukabiliwa na athari za kijamii na kiuchimi..
Mara nyingi viziwi huwa na vipato vidogovilivyo chini ya mstari wa umasikini , hawana rasilimali zinazoweza kutumika kukabili majanga, wana hali duni kijamii na kiuchumi, wana elimu duni, wana hali duni za afya na rishe duni,hawanufaiki na huduma na ulinzi wa kijamii, wanatengwa, wanabaguliwa na kunyimwa haki ya kutumia Lugha yao wenyewe.
Program hii inalenga kuongeza uelewa na matumizi ya Lugha ya Alama ya Tanzania (LAT)miongoni mwa viziwi na watu wasio na uziwi. program hii inaendeshwa kupitia utoaji wa mfunzo ya Lugha ya Alama,uratibu wa huduma za ukalimani wa Lughya Alama, kuendesha tafiti na uandaaji wa kamusi na nyenzo zingine.